Thursday, March 5, 2015

CHAMELEONE KUTIWA MBARONI KWA MAUAJI UGANDA

Staa asiyechuja kwenye anga za muziki, Jose Mayanja ‘Chameleone’ huenda akatiwa mbaroni kwa kuhusika katika kesi ya mauaji, baada ya baba wa kijana aliyefia kwenye mjengo wake, kuomba wahusika wa tukio hilo kuwekwa hatiani, kufuatia ‘umagumashi’ kujitokeza kwenye kesi hiyo.
Desemba 26, 2012, Chameleone alikumbana na msukosuko baada ya kijana mmoja; Robert Karamagi kuuwawa kwa kupigwa na kuchomwa moto eneo la nyumba yake lakini kesi hiyo haikupata muafaka baada ya kesi hiyo kufutwa kwa mamlaka ya Mwendesha Mashtaka (DPP).
Hata hivyo baba mzazi wa mtoto huyo Benedict Kyamanywa ambaye ni mwanajeshi mwenye cheo cha meja, juzi alilipua upya na kuomba mwendesha mashtaka (DPP) kutoa maelezo ya kina kuhusu jarida ‘file’ la kesi hiyo kutupiliwa mbali ilhali wahusika wakiwa hawajitiwa mbaroni mpaka sasa.
Mjeda huyo ambaye amerejea kutoka kwenye Somalia ambapo alikwenda kutuliza amani jana alifunguka: “Mauaji yaliyotokea mwaka 2012 wakati nikiwa Somalia, polisi waliniambia kuwa walikwenda kulifanyia uchunguzi na kuwatia nguvuni wahusika wote, lakini cha kusangaza nilipokwenda Makao Makuu ya Polisi Katwe, ambapo kesi ilikuwa ikisikilizwa, nilishutuka kuambiwa na Afsa mmoja kuwa file la kesi hiyo lilishafungwa na kuachana na suala hilo.”
Katika rufaa yake ya Feb 14, 2015 kwenda kwa DPP na nakala kwenda kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Gen. Kale Kayihura, Kyamanywa aliiomba DPP kuchunguza mazingira ya polisi kufunga kwa kesi ya mauaji ya mwanae na ikiwezekana kurejeshwa tena shaurini kesi yenyewe.
“Watu walioona tukio la mwanangu akipigwa na kuchomwa wapo na taarifa zilitunzwa. Hata wahusika katika mauaji hayo walirekodiwa na maelezo yao yapo kuwa walihusika. Chameleone mwenyewe alichukuliwa maelezo kuhusu tukio hilo na alisema kuwa mauaji yalitokea nyumbani kwake, kwa hiyo ninahitaji kujua sababu za msingi kwanini file lilifungwa,” alifunguka Maj. Kyamanywa. 
File ya kesi hiyo lililofunguliwa Katwe lilisomeka; KMP/E/01/2013.
Hata hivyo DPP, Richard Butera amesisitiza kuwa hakukuwa na kesi ya kujibu hivyo akaagiza kesi hiyo kufutwa. Alisema alifikia maamuzi hayo mwaka jana baada ya mapitio ya kesi na kujidhihirisha kuwa hakukuwa na kesi ya kujibu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.
“Tulikuwa na shahidi mmoja na tuliendelea nae kwa sababu alikiri kuona tukio hilo lakini baada ya kupitia, tulijidhihirisha kuwa shihidi wetu alikuwa amejichanganya katika maelezo yake.” Nikiri kuwa lilikuwa ni kosa kuwambia maofisa wangu kufuta kesi ile. Siku zote huwa tunawasiliana na waangwa wa kesi na kuwaeleza sababu za kufunga file lakini katika kesi hii, ni kweli hatukufanya hivyo.”

Chameleone matatani upya
DPP aliendelea kufunguka kuwa kutokana na kosa lao, wamelazimika kuifungua upya kesi hiyo baada ya shinikizo la Maj. Kyamanywa, ambaye ni baba wa marehemu.
“Kulikuwa na shahidi mwingine lakini ajuza sana ambaye alitaka kutoa ushuhuda lakini tulimshauri kwenda Polisi na kuja na ushihidi wa uhakika.”
Karamagi alikutwa akiwa amechomwa moto eneo la nyumba ya Chameleone, Desemba 2012 na alifariki muda mfupi baada ya kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mulago.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...