Thursday, March 12, 2015

AUNT EZEKIEL AKANUSHA TAARIFA ZA KUJIFUNGUA

Aunt Ezekiel.
BAADA ya kuzagaa taarifa za staa wa filamu nchini Aunt Ezekiel kujifungua, mwanahabari wetu ametia timu nyumbani kwa Aunt na kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mrembo huyo bado yu mjamzito na taarifa za kujifungua si za kweli.
Aunt akiwa na shosti wake Wema Sepetu.
Mitandao mbalimbali ya kijamii imeripoti taarifa za Aunt kujifungua kuanzia jana huku mingine ikimpongeza na kuweka kipande cha video kinachomuonyesha mwigizaji huyo akiwa ammbeba mtoto mchanga.

Aunt Ezekiel.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Aunt Ezekiel jana aliweka kipande cha video akiwa amembeba mtoto mchanga bila kuandika chochote.
Akiongea na mwanahabari wetu Aunt amesema kuwa , hicho ni kipande cha mojawapo ya filamu yake aliyocheza siku nyingi. Na taarifa zilizoenea mitandaoni kuwa kajifungua si za kweli.
Baadhi ya pongezi za mashabiki wa Aunt baada ya kuweka video inayomuonesha akiwa kambeba mtoto.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...