Monday, March 9, 2015

ANGALIA ORODHA YA MAGARI YENYE KASI ZAIDI DUNIANI


Ifuatayo ni orodha ya magari yanayotajwa kuwa na kasi zaidi duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Super Cars.Org, ndinga aina ya Hennessey Venom GT ndio mwisho wa maelezo na kinara wa spidi ambapo limeipiku Bugatti ambayo imekuwa kileleni kwa muda mrefu. NB mitandao nimetofautiana kwa kiasi fulani, orodha iliyotolewa na Top Car Rating ni tofauti.
Angalia list yenyewe kwa mujibu wa Super Cars. Org kwa mwaka 2014/15.


1. Hennessey Venom GT: 
Hukimbia km 435 kwa sasa. Thamani yake inakadriwa kuanzia dola milioni moja kwenda juu. Venom GT ndilo gari la kwanza kwa spidi ambapo ilijaribiwa tena Februari 14th, 2014 huko Florida, Marekani.


2. Bugatti Veyron Super Sport:
Kasi yake inatajwa kuwa km 431 kwa sasa huku kitita chake cha kulimiliki kikitajwa kuanzia dola milioni 2.4. Imekuwa kileleni katika magari yenye kasi duniani kwa kipindi cha miaka mitatu tangu
Julai 10, 2010, kwa sasa inashika nafasi ya pili baada ya jaribio lililofanyika Februari 14, 2014. 
Liliwahi kupoteza jina lake baada ya kufunikwa na SSC Ultimate Aero Machi, 2007 lakini mwaka 2010 hadhi yake ilirejea baada ya kuweka rekodi nchini Ujerumani  baada ya gari ain aya Super Sport kuibuka kinara wa mbio. Super ni kampuni ya Bugatti.
Lakini Bugatti original, yenyewe inatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 1.7



3. Koenigsegg Agera R:
 Kasi yake ni km 418 kwa sasa moja. Thamani yake ni kuanzia dola Mil. 1.6, hii ni hatari sana hususan maeneo ya barafu. Kwa sasa inatajwa kuwa adui mkubwa wa Bugatti, huku wataalam wakiamini ndani ya miaka mitano Bugatti inaweza kupata changamoto kubwa sana. 

HIZI ZINAFUNGANA #4.

4. SSC Ultimate Aero:
 Spidi yake ni km 413 kwa saa, sawa na mita 60 kwa sekunde 2.7. Bei yake ni kuanzia dola 654,400. Ilijaribiwa katika Machi 2007 katika rekodi za vitabu vya Guiness, wakati ikiibuka kinara kwa kipindi kuanzia mwaka 2007-2010.

4. 9ff GT9-R:
 Kasi yake ni  km 413 kwa saa  huku thamani yake ikitajwa kuwa  ni kuanzia dola 695,000.

5. Saleen S7 Twin-Turbo:
 Spidi yake ni km 399/ saa. Thamani yake inatajwa kuanzia dola 555,000 kupanda juu. Ina uwezo mkubwa wa kutembea umbali mrefu.


6. Koenigsegg CCX: 
Ni aina nyingine ya magari hatari. Hili lina uwezo wa kukata barabara kwa km 394 ndani ya saa moja ambapo bei yake inakadiriwa kuanzia kitita cha dola 545,568. Imetengenezwa nchini Sweden, ni ndugu na gari aina ya Agera R.

7. McLaren F1:
Inakula barabara km 386 ndani ya saa moja. Thamani yake ni kuanzia dola 970,000. Ndilo gari lilishika namba moja karne ya 20 ambalo milango yake imeundwa kama mabawa ya popo.

8. Zenvo ST1:
 Huwezi kutaja magari tishio kwa spidi usitaje Zenvo ST1. Ina uwezo wa kula barabara ya km 374 kwa saa. Thamani yake inaanzia dola Mil 1.25. Hili ni zao la Wadenishi.

9. Pagani Huayra:
Ina kata upepo wa km 370 ndani ya dakika 60! Injini yake ni kampuni ya Mercedes AMG. Thamani yake ni kuanzia pauni 849,000, au dola Mil. 1.27.

NAFASI YA 10 INASHIKWA NA MAGARI MAWILI.
10. Gumpert Apollo: 
Spidi yake ni km 362/ saa na thamani yake ikitajwa kuwa ni kitita cha dola 450,000. Imetengenezwa maalum kuwa na uwezo wa kupanda na kushuka na una unaweza kukunja kona ukiwa kwenye spidi ya  190 mph. 

10. Noble M600: 
Ina uwezo wa kukata km 362 ndani ya lisaa, lakini cha kuvutia zaidi ni kwamba thamani yake iko chini, kwani ni ya kitita cha dola 330,000 tu.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...