Tuesday, March 17, 2015

ANGALIA MAZISHI YA SYLVESTRE MARSH JIJINI MWANZA YALIVYOKAMILIKA



Jeneza lenye mwili wa marehemu Sylvestre Marsh likiingizwa kaburini kwenye makaburi ya Igoma, mkoani Mwanza.
 
MAJONZI, vilio na simanzi vimetawala wakati kocha wa zamani wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Sylvestre Marsh alipokuwa akiagwa leo na kisha kuzikwa katika makaburi ya Igoma, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Kocha Marsh alifariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akitokea Mwanza baada ya hali yake kuwa mbaya.

Mamia ya watu wakiwemo viongozi wa kiserikali, wadau wa soka, wanasoka na mashabiki wamehudhuria mazishi hayo yaliyoanzia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo ambapo marehemu Marsh na vijana wake walikuwa wakifanyia mazoezi.

Zoezi la kuaga mwili wa marehemu lilianza asubuhi katika uwanja huo baada ya mwili kuwasili kutoka katika Hospitali ya Seketule ulipokuwa umehifadhiwa.

Vijana waliokuwa wakifundishwa na Marsh katika Kituo cha soka cha Marsh Academy ndiyo waliopewa jukumu la kubeba jeneza la mwalimu wao.

Wanasoka wa zamani akiwemo Edibily Jonas Lunyamila na Fumo Felician ambao waliwahi kucheza soka na marehemu kabla ya kuwa kocha walimwaga machozi wakati wa zoezi la kumuaga mwenzao.

Wasanii wakiwemo Steve Nyerere na H-Baba nao wameungana na waombolezaji kumuaga mwalimu Marsh.

Sylvestre Marsh aliyezaliwa miaka 55 iliyopita, licha ya kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars tangu enzi za Marcio Maximo hadi Kim Poulsen, pia aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa zikiwemo Azam FC na Kagera Sugar.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiaga mwili wa marehemu Marsh.
Vijana walio katika Kituo cha soka cha Marsh Academy kilichokuwa kikiongozwa na marehemu wakishusha jeneza la mwalimu wao kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo tayari kwa kuaga.
Mke wa marehemu (wa pili kushoto) akilia kwa simanzi. Wa kwanza kushoto ni binti wa marehemu aitwaye Anna Marsh na kijana wake Wyne Marsh (wa tatu kushoto).
Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo viongozi wa serikali wakishiriki kumuaga marehemu Marsh.
Mmoja wa wadhamini wa kituo cha marehemu kutoka nchini Ujerumani akitoa salamu za rambirambi.
Nahodha wa timu ya vijana ya U-16 katika kituo cha marehemu akisoma historia ya Academy yao.
...Nahodha huyo akikakabidhi historia hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Sehemu ya waombolezaji waliohudhuria zoezi hilo.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...