Wednesday, February 4, 2015

KIPA WA SIMBA NDANI YA PENZI LA DEMU WA MJINI NAIMA


 
KIPA chipukizi wa timu ya Simba SC, Manyika Peter 'Manyika JR', anadaiwa kukamatika kwenye anga za mahaba ya mrembo wa mjini anayejulikana kwa jina la Naima, ambaye hivi karibuni aliwahi kuwa kwenye bifu zito na Wema Sepetu, akidai kumtaifisha bwana ake ajulikanaye kwa jina la CK.
Manyika amekuwa akionekana mara kwa mara akiwa na mrembo huyo na tukio la kushangaza ni usiku wa kuamkia Februari 3 mwaka huu ambapo Naima aliposti video katika peji yake ya Instagram akiwa na Manyika kwenye mkoko wake.
Manyika amekuwa akionekana na kudaiwa kutoka kimapenzi na mrembo huyo na sasa  imekuwa gumzo kwa watu wa karibu na wawili hao,
 Mara kadhaa pia Naima amekuwa akitamba na kuonyesha picha mbalimbali za mahaba akiwa na Manyika huku Manyika pia amekuwa akiendesha mara kadhaa gari la mrembo huyo aina ya Toyota Raum, na marafiki zake wakimtania kuwa sasa ameingia kwenye penzi la Mwarabu wa mjini.

Naima akiwa katika pozi na ujumbe ambao aliweka kwenye akaunti yake ya Instagram akijaribu kuwajibu baadhi ya watu waliokuwa wakimsema.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...