Tuesday, February 3, 2015

ALLY CHOKI KUUNGANA NA TWANGA PEPETA JUMAMOSI HII


BAADA ya wiki iliyopita Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki kupatanishwa na Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka, kufuatia ugomvi wao wa siku kibao, mapema leo Ally Choki ameahidi kuungana na bendi ya Twanga Pepeta jumamosi hii katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jiji Dar, katika Tamasha la Twanga Pepeta, lenye lengo la kusapoti onesho la miaka 16 Luizer Mbutu.
Luizer anafanyiwa onyesho maalum la kusherehekea miaka yake 16 tangu alipojiunga n bendi ya Twanga Pepeta bila kuhamia kwenye kundi jingine lolote kama ilivyokuwa ikifanywa na wasanii wengine wa dansi.
“Nitakuwepo Mango Garden kwa kazi maalum, lakini baadae nitarejea Meeda kuendeleza gurudumu la bendi yangu,” alisema Ally Choki.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...