Monday, February 2, 2015

AIRTEL KUWAPATIA TOYOTA ( IST) WATEJA WAKE KILA SIKU


Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bwana Levi Nyakundi (kushoto), akizindua promosheni kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku (kulia), ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Betrice Singano, uzinduzi huo umefanyika ndani ya Viwanja vya Maegesho ya Gari Mlimani City jijini Dar es Salaam, mapema leo.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya, akifafanua zaidi namna wateja wa Airtel watakavyoweza kujishindia gari kwa kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Yatosha.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya(wa kwanza kutoka kushoto), wakionyeshana ubora wa gari hizo na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Levi Nyakundi muda mfupi baada ya uzinduzi huo kumalizika.
 Msanii wa Bongo Fleva Nay wa Mitego (kulia), akionyeshwa moja ya magari yatakayoshindaniwa katika Promosheni hiyo.
 Mtangazaji wa Clouds FM, Mussa Hussein akiongea jambo kwenye uzinduzi huo.
 Baadhi ya waandishi wa habari na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini tukio hilo.

Airtel Tanzania leo imezindua promosheni  kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” promosheni hii ni nafasi ya peeke wa wateja wetu wanaojiunga na vifurshi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia. Nia yetu  kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora kwa kupitia huduma yetu ya Airtel Yatosha huku tukiwazawadia wateja wetu zawadi nono.
Tunaamini promosheni hii itawapatia wateja wetu uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma zetu za Airtel Yatosha. Zaidi ya wateja wetu kijishindia magari promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi itawapatia wateja wetu vifurushi zaidi “Aliongeza Nyakundi
Akiongea kuhusu namna ya kushiriki Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” ili kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya Yatosha vya siku, wiki na mwenzi.  hakuna gharama ya ziada, kwa kununua vifurushi vya yatosha tayari utakuwa umeunganishwa kwenye droo ya yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishinidia Toyota IST moja kila siku
Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha.  tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila siku”aliongeza  Mallya
Kununua vifurushi vya yatosha wateja wanaweza au  kupiga *149*99#, kunua kwa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha inayopatikana katika maduka yetu nchi nzima 
Mwaka Jana Airtel ilizindua huduma ya kisasa ya kibunifu na yenye vifurushi vya gharama nafuu sokoni. Kuzinduliwa kwa promosheni hii ya Airtel yatosha Zaidi ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora huku ikiwazawadia wateja wake kwa kutumia huduma zake

Mmoja wa washereheshaji katika uzinduzi huo akionyesha uwezo wa kuchezea pikipiki.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...