Wednesday, January 28, 2015

IVORY COAST, MALI ZAINGIA ROBO FAINALI AFCON 2015


 
Ivory Coast wakipongezana kwa ushindi dhidi ya Cameroon usiku huu.

TIMU za Mali na Ivory Coast nazo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa Afrika 2015 kutoka Kundi D huku Guinea na Cameroon wakiyaaga mashindano hayo.
Mali wamesonga mbele baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Guinea huku Ivory Coast wakiwachapa Cameroon bao 1-0. 
Kwa matokeo hayo Mali na Ivory Coast zimeungana na Ghana, Algeria, Congo, Equitorial Guinea, Tunisia na DR Congo katika hatua ya robo fainali. Katika hatua hiyo ya robo fainali, DR Congo watavaana na Congo, Tunisia na Equitorial Guinea, Ghana na Mali huku Algeria wakikipiga na Ivory Coast
 

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...