Friday, April 11, 2014

KABURI LA SHEIKH YAHYA HUSSEIN LAFUKULIWA

Kaburi la Sheikh Yahya Hussein ambaye alizikwa tarehe
21.5.2011.
Makaburi mawili ya Sheikh Yahya Hussein na Sheikh Kaseem Bin Jumaa yamevunjwa na mgambo wa jiji saa nane usiku eneo la Tambaza, makaburi ambayo yana muda mrefu katika eno hilo.

Hata hivyo haijajulikana chanzo cha kuvunjwa kwa makaburi hayo.

Wakiongea na waandishi wa habari baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya vyakula eneo hilo wamedai kuwa, walifika asubuhi na kukuta hali hiyo ya kuvunjwa kwa vibaraza vya maduka yao pamoja na kuvunjwa kwa makaburi hayo mawili ya watu masheikh mashuhuri hapa nchini.

Kaburi la Sheikh Kaseem Bin Juma ambaye alizikwa
mwaka 1994.

Naye mtoto wa marehemu Sheikh Yahya Hussein, Bi. Mariam Hussein alifika katika makaburi hayo na kujionea kwa macho yake jinsi kaburi la Baba yake lilivyobomolewa.

Mariam amesema anasikitishwa sana kwa kuvunjwa kwa kaburi la Baba yake bila ya sababu ya msingi.Mtoto wa Marehem Sheikh Yahya Hussein, Mariam Yahya
Hussein akitafakari jambo kwenye eneo
alilozikwa Baba yake mzazi.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...