Tuesday, March 11, 2014

YANGA SC. VS MTIBWA SUGER KUMENYANA JUMAMOSI HII NDANI YA JAMHURI MOROGORO

Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba SC na Coastal Union ya Tanga uliokuwa ufanyike kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umesogezwa mbele hadi Machi 23 mwaka huu.
Hiyo inafuatia Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kuifanyia marekebisho makubwa ratiba ya ligi hiyo ambayo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya Aprili 27 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

YANGA itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi 26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam Complex).
Machi 29 mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino (Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal vs Mgambo (Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT Ruvu (Taifa).
Aprili 12 mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini), Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa).
Wakati huo huo: Marefa na marefa wasaidizi 22 wameteuliwa kushiriki semina na mtihani wa utimamu wa mwili kwa robo ya kwanza ya mwaka huu itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 14 hadi 16.
Semina hiyo inashirikisha waamuzi wote wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu (elite) kutoka Tanzania Bara za Zanzibar.
Waamuzi hao ni Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama (Iringa), Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya) na Jonesia Rukyaa (Bukoba).
Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza Kinduli (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Wakufunzi wa semina hiyo ambao wanatambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Joan Minja na Riziki Majala.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...