Friday, March 7, 2014

NGONO NJENJE KWENYE VIGODORO VYA USWAZI.Jiji la dar es salaam huwa ni tamu lakini lina kero zake na uenda kero ni nyingi kuliko raha zilizopo… moja wapo ya kero kubwa zaidi ni hili ambalo bila shaka kila mmoja wetu anayeishi uswahilini linamgusa kwa namna moja ama nyingine … si linguine ni swala hili la miziki ya kukesha ambayo imejichukulia umaarufu kwa jina la vigodoro, kwa mtu anaye kaa mitaaa ya mbezi beach, upanga au masaki ni vigumu kuelewa nachomaanisha lakini kwa watu wa yombo vituka, tandale kwa tumbo , ukonga mazizini na sehemu kama tandika wananielewa vizuri…

Ni ukweli usiopingika kuwa hii ni kelo ya watanzania wengi hapa jijini, mara nyingi miziki hii uanza siku ya alhamisi au ijumaa na kwenda mpaka jumapili… kero hii inatokana na mtindo wa upigaji wa mziki huu usiozingatia mda ambapo upigwa mpaka asubuhi bila kujali usumbufu mkubwa wanoupata watu wa karibu na vigodoro hivyo…sasa pata picha umerudi toka kazini sa tano usiku kutokana na foleni iliyopo mjini na unaamua kujipumzisha kidogo ili uwahi kuamka ukatafute riziki… kwa sauti ya mziki huu sidhani kama utapata usingizi … kitu ambacho kinaweza kupelekea uamke umechoka na ushindwe kufanya kazi zako kwa ufasaha,,,, hapa tunaweza kusema kwamba miziki hii inarudisha nyuma maendeleo ya watanzania nan chi kwa ujumla. Kero nyingine ya miziki hii ya usiku ni ukiukwaji wa maadili ya mtanzania kwani kubali ukatae watu wanacheza bila kuhofia chochote na mara nyingi kama unavyojua nyumba zetu za uswahilini wengi hatuna mageti ya kuwazuia watoto wetu… watoto wengi wa umri wa chini ya miaka kumi na nane wamekuwa wakitoroka nyumbani na kukimbilia kwenye vigodoro hivo na kuwafanya wajifunze tabia ambazo ni zaidi ya umri wao.
Nadhani imefika wakati sasa serikali kuangalia upya sharia za upigaji mziki katika kumbi za starehe na majumbani.. mara nyingi sharia inasema baa zifungwe sa sita labda uwe na kibali naalum kutoka sehemu husika .. lakini hii imekua ni tofauti kwa vigodoro kwani uenda mpaka asubuhi na kusababisha kero isiyokuwa ya kawaida kwa wakazi wa maeneo ya uswahilini

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...