Tuesday, March 11, 2014

MRISHO NGASSA AZUIWA KUFANYA MAZOEZI YANGA
Mchezaji wa Timu ya Yanga Mrisho Ngassa wa kwanza kutoka kushoto akiwa nje ya uwanja asubuhi ya leo,mara baada ya kukatazwa kushiriki mazoezi ya pamoja na wenzake kwenye uwanja wa timu ya Al Ahly,anayemfuatia katikati ni msemaji wa timu hiyo Baraka Kizuguto na mwisho ni Mganga wa Timu hiyo Juma Sufiani.


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ameendelea kukaa nje bila ya kufanya mazoezi kutokana na daktari wa timu hiyo kuona hayuko fiti.

Daktari wa Yanga, Juma Sufiani amesema bado hajawa katika kiwango cha kujumuika na wenzake baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Al Ahly.
 


“Bado hajawa katika hali nzuri, sasa anaendelea na matibabu, hivyo naweza kusema bado hajawa fiti,” alisema.


Ngassa alitolewa wakati wa mechi hiyo juzi kwenye Uwanja wa Max jijini Alexandria baada ya kuumia.


Katika mechi hiyo, Yanga ililala kwa mikwaju ya penalty 4-3 na kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

HABARI/PICHA:SALEHJEMBE BLOG

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...