Friday, February 28, 2014

KUELEKEA BONANZA LA JOGGING DAR LIVE, ACB, WARATIBU WAWEKA WAZI MIKAKATI YAO







Meneja Masoko wa Global Publishers, Innocent Mafuru (kushoto) akiwatambulisha wageni waliofika ofisi za Global Publishers kuelezea maandalizi ya Bonanza la Jogging litakalofanyika Dar Live Jumapili hii.


Kutoka kushoto ni waratibu wa Bonanza la Dar Live, Rajab Mteta 'KP', Mshauri Barandu wakiwa na Mkuu wa Masoko wa Akiba Commercial Bank (ACB), Innocent Ishengoma.


Mhariri Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Richard Manyota akiwakaribisha wageni Global.


Mkuu wa Masoko wa Akiba Commercial Bank (ACB), Innocent Ishengoma akiongea na wafanyakazi wa Global (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kulidhamini Bonanza la Jogging Dar Live.


Mratibu wa Bonanza la Dar Live, Rajab Mteta 'KP', akieleza mikakati waliyonayo kuelekea Bonanza la Jogging Jumapili.


Mratibu wa Bonanza la Dar Live, Mshauri Barandu akiongea na wanahabari (hawapo pichani).


Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Amran Kaima akiuliza jinsi waandaaji walivyojiandaa katika Bonanza la Jogging.

Mwakilishi wa mmoja wa wadhamini wa Bonanza la Jogging litakalofanyika Dar Live Jumapili hii, Innocent Ishengoma kutoka Akiba Commercial Bank (ACB), pamoja na waratibu wa bonanza hilo leo wametembelea ofisi za Global Publishers Ltd kuelezea walivyojipanga kuelekea katika bonanza hilo litakalofanyika ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakheem, Dar.

Bonanza hilo ambalo hukusanya maelfu ya wanajogging jijini Dar limedhaminiwa pia na Mfuko wa Pensheni (PSPF) na Damu Salama.

(PICHA NA ERICK EVARIST / GPL)

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...