Thursday, January 23, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWASILI KWENYE DARAJA LA DUMILA MVOMERO-MOROGORO


Daraja la Dumila wilayani Mvomero, Morogoro likiwa limekatika baada ya kunyesha mvua kubwa.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda hivi punde amewasili eneo la daraja la Dumila mkoani Morogoro lililokatika baada ya kunyesha mvua kubwa ili kujionea hali halisi ya eneo hilo pamoja na kutoa pole kwa familia zilizokumbwa na maafa hayo.

Mhe. Pinda ametua kwa helkopta ya polisi na ameungana na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli aliyetangulia eneo hilo. Mpaka sasa hakuna magari yanayopita eneo hilo kutokana na kukatika kwa daraja hilo ambalo ni kiunganishi kati ya mkoa wa Dodoma na Morogoro

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...