Tuesday, January 14, 2014

RAIS WA TFF JAMAL MALINZI KUFUNGA SEMINA YA WAAMUZI LEO



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa semina ya waamuzi na makamisha leo (Januari 4 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


WAAMUZI zaidi ya 100 na makamishna 50 wameshiriki katika semina hiyo. Makamishna hao ni baadhi ya wale wanaosimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati waamuzi ni wale wa daraja la kwanza (class one) ambao ndiyo wanaochezesha mechi za VPL na FDL.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kuandaa semina nyingine baadaye mwaka huu kwa makamishna wapya wanaotaka kusimamia mechi za VPL na zile za FDL.

HABARI/PICHA:  SALEHJEMBE BLOG

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...