Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.
Wakili wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.
Aidha Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa Zitto Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.
Tundu Lisu akiwatuliza na kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa kichwani kwa jiwe.
No comments:
Post a Comment