
Mtangazaji wa Kipindi cha XXL Hamisi Mandi 'B12', akiwa katika pozi
WATANGAZAJI Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, hatimaye leo wameanza rasmi kuchapa kazi yao ya utangazaji baada ya kurejeshwa kwa mara nyingine kazini hapo kufuatia kusimamishwa na uongozi wa Clouds Media Group kwa takribani wiki tatu zilizopita,Watangazaji hao waliingia kwenye mgogoro na uongozi huo baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano na waajiri wao na kupelekea kuwapa adhabu hiyo, nakuwafanya wawe nje ya chumba cha kurushia matangazo ya redio hiyo, pamoja na kusimamishwa pia walitakiwa kuripoti kazini kila siku hadi leo ambapo wamesamehewa na kuanza kusababisha burudani kama ilivyokuwa mwanzo


Adam Mchomvu akitabasamu kwa pozi
No comments:
Post a Comment