Friday, January 24, 2014

ANGALIA WABONGO WALIVYO WATAALAMU WA KUAGIZA VITU POPOTE UENDAPO KWENYE DUNIA HII


WABONGO KWA KUAGIZA TU HAWAJAMBO
Wabongo bwana..! Kila mji utakaokwenda hawakosi chakukuagiza. Kama waenda Mbeya utasikia, "Tuletee maparachichi na mchele." Ukienda Moshi unaagizwa, "Usisahau kutuletea kahawa."
Ukienda Dodoma utasikia, "Utuletee zabibu na karanga."
Ukienda Tabora wapo tu, "Pliiiiz utununulie asali huko."
Ukienda Morogoro wanaagiza, "Tuletee magimbi basi."
Ukienda Bagamoyo utaagizwa, "Mananasi ya kule matamu usisahau kutuletea."
Ukienda Tanga utasikia, "Tuletee machungwa jamani!"
Ukienda Songea, utasikia "Usisahau viazi vyaSongea."
Ukienda Mtwara utaagizwa, "Tuletee korosho unaporudi."
Ukienda Kigoma, "Jamani rudi na mafuta ya mawese na migebuka."
Ukienda safari inaishia Singida wana wewe tu, "Basi utuletee mafuta ya alizeti."
Ukiwaambia unakwenda Mwanza wanaagiza, "Utuletee samaki sana sana Sato."
Kama waenda Bukoba hawachoki tu, "Tafadhali utuletee senene."
Kasheshe sasa kama safari yako inaishia Iringa.Utasikia sasa, "Niletee mdada wa kazi jamani!"

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...