Friday, December 27, 2013

TAMASHA LA KRISMAS LILIVYOBAMBA MJINI MOROGORO LEO



Mmoja ya Waimbaji machachari katika anga ya muziki kiroho a.k.a Injili,Bone Mwaitege akionesha umahiri wake wa kucheza,na madansa wake kwenye uwanja wa Jamuhuri,mkoani Morogoro mapema leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Krismasi,ambapo hapo jana limezinduliwa rasmi jijini Dar katika uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watu kibao.

Mwimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu,Upendo Kilahiro akiwaimbisha sehemu ya wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kwenye muendelezo wa tamasha la krisimasi lililofanyika jioni ya leo ndani ya uwanja
wa jamuhuri mkoani Morogoro.

Madansa wa mwimbaji nyota wa muziki wa Injili hapa nchini,Rose Muhando wakiwajibika vilivyo.
Malikia wa nyimbo za Injili,Rose Muhando akiimba kwa hisia wimbo wake mpya uitwao FACEBOOK,ndani ya uwanja wa jamuhuri,mkoani Morogoro mapema leo jioni.

Sehemu ya mashabiki wakishangilia.
Mwimbaji wa injili kutoka nchini Zambia,Eprahim Sekereti akiimba sambamba na kundi la Victoria singers,ndani ya uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro jioni ya leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Krisimasi.

Mwimbaji wa nyimbo za injili,Upendo Nkone akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani) waliofika kulishuhudia tamasha hilo la mwendelezo wa krisimasi mpaka mwaka mpya.

Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za kiroho kutoka mkoani Morogoro,Tumaini Njole akiimba huku akiwa katika staili ya kipekee kabisa,huku mayowe na shangwe zikisikika kutoka kwa mashabiki


Sehemu ya mashabiki

Vijana wa kundi la The Voice wakiwaimbisha mashabiki na watazamaji waliofika kwenye tamasha hilo ndani ya uwanja Jamuhuri mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...