Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
AWALI ya yote, nianze kwa kumshukuru sana Mungu wa mbinguni kwa jinsi anavyoendelea kutenda miujiza katika maisha yetu. Kila kinachotutokea ni kwa sababu yake na hakuna lolote ambalo tunaweza kumlaumu zaidi ya kumshukuru kwa vile kila jambo linakuja kwa sababu maalum.
Baada ya angalizo hilo, naomba sasa nije moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo. Miezi michache iliyopita, tunakumbuka kwamba taifa lilitangaza oparesheni maalum ya kutokomeza ujangili, ikiwa na lengo la kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watu wote waliokuwa wakijihusisha na uwindaji haramu, kiasi cha kuhatarisha uwepo wa wanyama, hasa tembo na faru.
Ni oparesheni kubwa iliyolenga siyo tu kuwaokoa wanyama na kukomesha vitendo hivyo vya ukiukwaji wa sheria, bali pia ilikuwa na nia ya kutokomeza kabisa mtandao huo, unaodaiwa kuwa mkubwa, ndani na nje ya nchi.
Katika utekelezaji wake, serikali iliamua kutumia nguvu kubwa, kwa kuyaingiza katika oparesheni hiyo majeshi yetu (Polisi na JWTZ), viongozi wa kaya zinazoishi karibu na maeneo ya hifadhi, askari wa wanyama pori na watu wengine wote ambao waliaminika kwa njia moja au nyingine, watasaidia kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Lakini katika hali ya kusikitisha, vijana hawa wanaolipwa mishahara kwa kodi za wananchi, waligeuka na kuharibu maana nzima ya zoezi hilo, kiasi cha kusababisha uharibifu mkubwa wa mali, udhalilishaji wa hali ya juu pamoja na dhuluma kwa watu.
Badala ya kuwasaka majangili na kuwatokomeza, watu waliingia katika vijiji na kuvichoma moto bila sababu za msingi, kuwabaka akina mama, kuwapora fedha, mifugo na wakati mwingine kusababisha mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia.
Ulikuwa ni unyama wa hali ya juu ambao Watanzania waliwafanyia Watanzania wenzao katika namna ambayo inasikitisha sana. Wananchi kupitia kwa wawakilishi wao bungeni walilalamikia zoezi hilo na kwa kauli moja, bunge likaridhia kusimamishwa kwa oparesheni hiyo, ili kulipa nafasi ya kufanya uchunguzi na kuja na majibu.
Kamati ya bunge iliyoundwa kuchunguza tukio hilo, iligundua kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa maadili na haki za binadamu, hali iliyowafanya mawaziri watatu kutakiwa kuachia ngazi na mmoja kutangaza kujiuzulu muda mchache kabla ya waziri mkuu kutoa tangazo hilo la kuwasimamisha bungeni.
Huu ni uamuzi ambao ulipaswa kuchukuliwa hasa ukiangalia unyama waliofanyiwa watu ambao hawakuwa walengwa. Lakini wakati hali imetokea hivi mawaziri hawa, ambao wamewajibishwa kwa kitendo cha kutowasimamia vizuri walio chini yao, nadhani sasa lazima upande wa pili wa shilingi uangaliwe, uchunguzwe na hatua zichukuliwe.
Hawa waliohusika katika kuwabaka mama na dada zetu, waliojichukulia sheria mikononi na kupora mifugo ya wafugaji, kuchoma moto nyumba na vyakula vya wananchi, kuwatesa, kuwadhalilkisha na hata kuwasababishia vilema vya kudumu na vifo, ni lazima washughulikiwe kisheria.
Tutakuwa hatutendi haki kwa Watanzania kama tutawaacha watu hawa waendelee na maisha yao wakati wamefanya ukatili mkubwa kwa wananchi. Kwa sababu wanafahamika ni lazima wafikishwe mahakamani kwa mashtaka wanayostahili ili haki itendeke.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli!

No comments:
Post a Comment