Monday, December 16, 2013

PETER O’TOOLE WA ‘LAWRENCE OF ARABIA’ AFARIKI AKIWA NA MIAKA 81


Peter O'Toole enzi za uhai wake.

MCHEZA sinema Peter O'Toole, aliyeng’aa mnamo mwaka 1962 alipocheza kama T. E. Lawrence katika filamu ya "Lawrence of Arabia", amefariki akiwa na umri wa miaka 81, shirika la BBC limetangaza. O'Toole, alifariki Jumamosi iliyopita (Desemba 14) katika Hospitali ya Wellington, jijini London, baada ya kuugua kwa muda mrefu, jambo ambalo lilithibitishwa na wakala wake, Steve Kenis.

Mwigizaji huyo, mzaliwa wa Ireland, aliyetangaza kuacha sanaa hiyo, aliwahi kushinda tuzo zinazojulikana kama Academy Awards kwa kucheza katika filamu za "Lawrence of Arabia," "Becket" (1964), "The Lion In Winter" (1968), "Goodbye, Mr. Chips" (1969), "The Ruling Class" (1972), "The Stunt Man" (1980), "My Favorite Year" (1982) na "Venus" (2006).

Pia alishinda tuzo nne za Golden Globes, BAFTA na ya Emmy, mbali na kushinda tuzo ya heshima iliyojulikana kama Honorary Academy Award mwaka 2003.

O'Toole ameacha mabinti Kate na Patricia, na mtoto wa kiume Lorcan.

Picha na: Popperfoto/Getty Images

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...