Friday, December 20, 2013

KIMENUKA BUNGENI WAZIRI MKUU,KAGASHEKI,NCHIMBI NA SHAMSI VUI NAHODHA WABUNGE WAWATAKA WAJIUZULU LEO DODOMA


 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
WABUNGE wamewataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu kutokana na maovu yaliyofanywa wakati wa Operesheni Tokomeza wakati wakijadili ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.

Baadhi ya wabunge waliochangia kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri hao ni Mbunge wa Mwibara (CCM) Kangi Lugola, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Longido (CCM) Lekule Laizer.

Bunge litaendelea kujadili ripoti hiyo saa 10 jioni.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...