Tuesday, December 24, 2013

BARAZA LA USALAMA BARABARANI LAHAMASISHA USALAMA WA RAIA MSIMU HUU WA CHRISMASI NA MWAKA MPYA



Kampuni ya mitandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza ushirikiano wake na Baraza la Taifa la Usalama barabarani katika juhudi za kuelimisha uma kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani hususani msimu huu wa sikukuu.

Airtel imekuwa ikishirikiana kwa karibu na kikosi cha Usalama Barabarani katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kudhamini kampeni mbalimbali. 
 
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia) akisisitiza juu ya umuhimu wa wananchi kujikinga na ajali za barabarani kwenye msimu huu wa sikukuu leo wakati wa kikao na waandishi wa habari kilichofanyika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akifuatiwa na Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi.Hawa Bayumi alisema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wananchi wanapaswa kuwa waangalifu zaidi ili kujikinga na ajali za barabarani.


“Hiki ni kipindi ambacho wananchi wanapaswa kuwa makini sana katika kuhakikisha wanajilinda na wimbi la ajali za barabarani ambazo husababisha asara kubwa kwa taifa, na pia madereva wajitaidi sana kuepuka ulevi wa kupindukia,” alisema Hawa.



Aliongeza kwa kusema pia katika msimu huu wateja wa Airtel wanaweza kutumia huduma ya Airtel money kutuma na kupokea pesa bure mahali popote nchi nzima kuepuka kutembea na viwango vikubwa vya pesa.

Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya umuhimu wa kujikinga na ajali za barabarani katika msimu huu wa sikukuu pia kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake wananchi watumie huduma ya Airtel money. Kushoto kwake ni Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi pamoja na Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam leo. DCP Mohammed Mpinga alisema Lengo la kampeni hizi ni kupunguza ongezeko la ajali za barabarani pamoja na madhara yake kwa kipindi cha sikukuu za mwaka huu 2013/2014 na wanajitaidi kuhakikisha elimu inatolewa ipasavyo.


“Tunashukuru Airtel kwa kuungana nasi katika kujali usalama wa watanzania, kazi ya kuelimisha watumiaji wa barabara ni kubwa na hivyo tunaendelea kutoa wito kwa wadau wengine kutuunga mkono ili kusaidia kufikisha ujumbe. Lengo hili litatimia kwa kushirikiana na wadau katika kufanya operasheni mbalimbali pamoja na kutoa elimu.” Alisema DCP Mpinga.



Mpinga alitumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania wote kote nchini kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake watumie huduma ya Airtel Money kutuma, kuweka na kutoa pesa.

Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi akizungumzia athari zinazotokana na ajali za barabarani na kuwaasa wananchi waziepuke hususani katika msimu huu wa sikukuu. Bw. Athumani Hamisi alisema Kuelekea mwisho wa mwaka, matukio ya ajali za barabarani yamekuwa yakiongezeka kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani hivyo wananchi wanatakiwa kujitahidi kutokiuka taratibu hizo.


“Ukiukwaji wa sheria husababisha sana ajali za barabarani, wananchi wanapaswa kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kuepusha ongezeko la ajali hizo ambazo hutokea mara kwa mara haswa katika msimu huu wa sikukuu.” Alisema Athmani.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...