Wednesday, December 18, 2013

ANGALIA JOKATE ALIVYOZINDUA KIDOTI CLUB



Pichani kulia ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006,Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali mapema leo Mikocheni jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa klabu yake iliyojulikana kwa jina la KIDOTI CLUB,Shoto ni mmoja waratibu,Mtangazaji wa East Africa Radio aitwaye Bhoke.

Mmoja wa Mashuhuda akitoa ushuhuda wake mara baada ya kujiunga kwenye klabu ya KIDOTI CLUB,kwa njia ya simu kwa kutuma neno KIDOTI kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.


Baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo uliofanyika Mikocheni,jijini Dar.


========= ======== ========


Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club.

Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jana, Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali katika jamii hususani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand.

Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti. Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye.

Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.

“Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii,Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi. Alisema kuwa pia ataendesha mashindano mbali mbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.

“Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji chake kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu name kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote, natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbali mbali ya maisha,” alisema.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...