Thursday, November 28, 2013

ATUHUMIWA KUMUUA BOSS WAKE KWA KOSA LA KUULIZWA UMECHELEWA WAPI!






Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula (32)ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani mbeya akiwa chini ya polizi kwenda kuonyesha pesa na simu alivyotumbukiza chooni

Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula (32)ambaye alikuwa akiishi naye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani mbeya

Daniel alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi, Pelesi lijulikanalo kwa jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya.

Chanzo cha ugomvi inadaiwa kuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo Pelesi alipochukua jukumu la kumuuliza jambo lililozua ugonvi katiyao na kusababisha kifo cha bi.Pelesi Chaula.

Kifo cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali mwilini mwake.

Wakati mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini wilayani Makete mkoani Iringa.

Baada ya mauaji hayo Kijana Daniel alichukua simu mbili za marehemu na simu yake pamoja na fedha kiasi cha 114000/= na kuzitumbukiza chooni kisha alienda kwa jirani kuwajulisha kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na kwamba wamemuua bosi wake huyo.

Majirani walipofika eneo la tukio walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya nyumba iliyokuwa imevunjwa, walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau kufunga milango, baaada ya majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua kutoa taarifa polisi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi,Neema Mwasampeta alisema,' Dan alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani hicho ndiyo chanzo cha ugomvi wao'. aliongeza kuwa alimjua kijana huyo kwa muda wa mwaka mmoja.




Marehemu Bi,Pelesi Chaula (32) enzi za uhai wake



Harakati za kutafuata fedha na simu tatu zilizotupwa chooni na anaetuhumiwa kwa mauaji

Afisa upelelezi wa wilaya Mbeya mtatiro akishukuru wakazi wa mtaa wa iyela kwa ushirikiano utulivu waliouonyesha wakati wa zoezi la kutafuta vidhibiti.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...