Wednesday, October 2, 2013

'AUNT EZEKIELI, WEMA WADAIWA KUONYESHA KUSAGANA CHINA'



LICHA ya mwaka jana kuita vyombo vya habari na kujisafisha baada ya kukaa nusu utupu jukwaani, mastaa wawili wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel wamefanya uchafu wakiwa Hong Kong, China.
Video ya aibu ya wawili hao ilivuja mitandaoni mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwaonesha ‘wakidendeka’ na kufanyiana vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
Video hiyo inaonesha ilirekodiwa siku ya ‘bethidei’ ya Wema, Septemba 27, mwaka huu ambapo bidada huyo alikuwa akitimiza umri wa miaka 25.
Katika video hiyo waliyorekodi wakiwa China, wawili hao wanaonekana kwenye chumba wakiimba wimbo wa ‘Happy Birthday’ na baada ya kumaliza, wakasogezeana midomo na kumwagiana mabusu ya nguvu.
Uchafu zaidi unaonekana pale Aunt alipojisogeza kwa Wema na kukutanisha midomo kisha kudendeka wakati wakipongezana.
Kwa mujibu wa mashabiki wao walioiona video hiyo, wasanii hao wanatakiwa kutambua kwamba wao ni kioo cha jamii huku Aunt akipondwa zaidi kwa kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte.
Mwaka jana Wema na Aunt waliangua vilio mbele wa wanahabari walipokuwa wakiomba radhi kwa kukaa nusu utupu jukwaani kwenye Tamasha la Fiesta lakini kinachoonekana wamekuwa sikio la kufa lisilosikia hata kama likipatiwa dawa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...