Friday, September 13, 2013

SERENGETI FIESTA KAMATA FURSA TWENZETU YAWASISIMUA VILIVYO WAKAZI WA DODOMA

KAMPENI mpya ya Serengeti Fiesta Kamata Fursa Twenzetu 2013, leo imewasisimua vilivyo baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria katika semina ya kujifunza namna ya kutumia fursa za sehemu husika kwa kujikwamua kimaisha, iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa  African dream.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mtahaba,akiongea jambo mbele ya wakazi wa Dodoma waliyojitokeza kwenye Semina hiyo ya Kamata fursa Twenzetu ndani ya Ukumbi wa African Dream mjini Dodoma.

 Millard Ayo akiwa katika pozi na moja ya mashabiki wake waliokuwa katika Semina ya Kamata Fursa Twenzetu ndani  ya Ukumbi wa African Dream mjini Dodoma mapema leo
Mwakilishi wa NSSF kutoka Makao Makuu Salim Khalifan akifafanua jambo kwa wakazi wa Dodoma na kuwaelekeza namna ya kutumia Fursa katika kujikwamua kimaisha hasa kupitia mikopo mbalimbali inayotolewa na  NSSF.

Meneja Masoko wa  Maxcom African Bernard  Munubi akiwafafanulia wakazi wa Dodoma namna wanavyoweza kuitumia bidhaa ya Max Malipo katika kujikwamua kimaisha.
Mmoja wa wakazi wa Dodoma aliyesimama kulia akiuliza swali kutokana na uelewa wake katika semina hiyo.
Bwana Shamba  Yona Joram akiwafafanualia wakazi hao namna ya kutumia fursa ya kujikwamua kimaisha katika sekta ya kilimo.

Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa Twenzetu, iliyounguruma mapema leo ndani ya Ukumbi wa African Dream mjini Dodoma

Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa Twenzetu, iliyounguruma mapema leo ndani ya Ukumbi wa African Dream.

Ruge
 Millard akiwa katika pozi na watu wake wa nguvu muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina ya Kamata Fursa Twenzetu.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma  Kirondera Nyabuyenze (kulia),naye alipata fursa ya kuongea na  wakazi wa mkoa wake kutoka kwa Mtangazaji wa Clouds FM, Jerald Hando aliyesimama kushoto .
Mtangazaji wa Clouds Media Group Millard Ayo akiwapa mbinu za kutokata tama kimasha wakazi wa Dodoma kwa kuwasimlia yeye alikotokea hadi kufikia nafasi aliyonayo leo hii.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...