Saturday, September 28, 2013

LULU AWAONYESHA FURSA WAKAZI WA MWANZA LEO

 Msanii wa Filamu Bongo,Lulu akiongea jambo na wakazi wa Mwanza kwenye Semina ya Kamata Fursa Twenzetu ndani ya Ukumbi wa Golden Crista mapema hii
Lulu akipokea pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh.Steven Masele muda mfupi baada ya kushuka jukwaani kuzungumzia mambo ya Kamata Fursa Twenzetu
Naibu Waziri wa Madini, Mh. Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest, Bw. Mathias Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini, aliyajipatia fursa mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.


Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kusubiri Serikali iwafanyie ama iwaletee kila kitu hapo walipo.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Januari Makamba akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina, sambamba na fursa ya matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu,iliyofanyika leo,ndani ya ukumbi Gold Crest, jijini Mwanza.

Sehemu ya wakazi wa mji wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzetu,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada mbalimbali zilikuwa zikizungumzwa.

Mmoja wa wasanii wa bongofleva, Nikki Wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twendzetu.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max Malipo, Bw. Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya Max Malipo inavyoweza kuisadia jamii kwa namna moja ama nyingine.

Baadhi Washiriki wakifuatilia.

Mmoja wa waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael "Lulu" akiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest, jijini Mwanza asubuhi hii,ambapo pia atazungumzia mambo kadhaa mbalimbali kwenye semina hiyo, ambayo itawakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Januari Makamba, Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini na watoa mada wengine mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Bi. Magreth Chacha alipokuwa akiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu, ndani ya ukumbi Gold Crest, jijini Mwanza asubuhi hii.

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Mh. Januari Makamba akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele (mwenye miwani) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha walipokuwa wakiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu, ndani ya ukumbi Gold Crest, jijini Mwanza asubuhi hii,pichani kati ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group, Bw. Ruge Mutahaba.


Baadhi ya Wakazi wa mji wa Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu, ndani ya ukumbi Gold Crest, jijini Mwanza asubuhi hii.

Sehemu ya meza kuu.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...