Thursday, September 12, 2013

DIAMOND KUANZIA LEO SITAKI COLLABO NA MSANII YOYOTE



JANA Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo,Nasib Abdul alipata fursa ya kuzungumzia madai yaliyokuwa yakitolewa na wasanii wenzake wa Bongo Fleva Dayna Nyange na Baba Revo yaliyohusiana na tuhuma za kutumia biti ya wimbo wake mpya kimakosa,
 Diamond hakupata nafasi ya kulizungumzia suala hilo kutokana na kubanwa na shughuli zake za kimuziki ila jana alipata nafasi na kuongea mengi ila jambo la msingi aliloongea ni pamoja na kukataa kufanya tena collaborate na wasanii wenzake hasa wasio eleweka kisanaa.
akifafanua zaidi alisema katika kipindi cha   XXL baada ya kuulizwa na Mtangazaji wa kipindi hicho B12aliyekuwa studio hapo na  Adam Mchovu waliyomuuliza swali la kwamba anaamua nini na anajiskiaje kila anapotoa wimbo watu wanamlalamikia kwakusema kawaibia?
 Diamond alijibu kwa kusema kuwa  kuanzia sasa hivi hataki collabo na
msanii yeyote wa bomgo fleva isipokuwa atafanya na baadhi  ya wasanii  anaoheshimiana nao tu.
,kwani amegundua swala hilo ndilo linalosababisha matatizo kama yanayotokea kwa baadhi ya wasanii anapotumia vibaya nafasi hiyo kwa kuzusha kuwa wameibiwa wimbo au beat zaona hasa lengo lao wengi wanakuwa wakitafuta kiki tu.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...