Sunday, August 25, 2013

RAGE NDANI YA BURUNDI KUCHUKUA ITC ZA TAMBWE,DEMUNGA


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage yuko mjini Bujumbura kufanya juhudi za kupata ITC za wachezaji wawili, Kaze Patrick ‘Demunga’ na Amis Tabwe.
Wachezaji hao walishindwa kucheza mechi ya jana wakati Simba ilipoivaa Rhino ya Tabora na kutoka sare ya mabao 2-2.
Kutokana na hali hiyo, Rage amefunga safari hadi Burundi ili kuhakikisha suala hilo linafanikiwa.
“Kweli Rage yuko Bujumbura kupambana na hili suala, kidogo Warundi wanataka kutufanyia kitu ambacho si sahihi. Wanasema wana mikataba na hao wachezaji, lakini hawataki kuionyesha kwa kuwa wachezaji wenyewe wanasema hawana mikataba na Vital’O,” alisema mpasha habari.
Awali imeelezwa kuwa, Shirikisho la Soka la Burundi linataka kufanya njama ili kuhakikisha wanabaki kuwa wachezaji wa Vital’O ili liwatumie katika michuano ya Chan nchini Afrika Kusini kwa kuwa Burundi imefuzu.
Burundi ilifuzu katika michuano hiyo kwa kuwatoa Sudan na wachezaji hao walikuwa sehemu ya chachu ya ushindi huo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...