Saturday, August 31, 2013

LULU AZINDUA FOOLISH AGE MLIMANI CITY


 
MSANII wa Filamu Bongo Elizabeth Michael 'Lulu' akiongea jambo mbele ya waarikwa na mashabiki zake waliyohudhuria mahali hapo muda mfupi kabla ya uzinduzi wa movie yake ya Foolish Age kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judithi Wambura 'Lady Jaydee akitoa burudani kwa mashabiki waliyohudhuria uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ndani ya  Ukumbi wa Mlimani City.

Msanii wa Bongo Fleva Elias Barnaba 'Barnaba Boy', naye alipata fursa ya kutoa burudani kwenye uzinduzi huo.

Mzazi wa marehemu Steven Kanumba akiangua kilio huku akiwa amekumbatiana na Wema Sepetu,muda mfupi baada ya kukutana kwenye shughuli ya uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Dar.

Baadhi ya mashabiki na wapenzi wa burudani wakiserebuka na nyimbo hatari za Machozi Bendi,zilizokuwa zikiimbwa na Lady Jaydee katika uzinduzi wa filamu hiyo.
 
Lady Jaydee,Gardener kulia wakiwa kwenye meza ya pamoja na waratibu wa uzinduzi huo.

  Josephat Lukaza akiwa katika pozi  na mrembo mmoja anayetambulika kwa jina la Fetty



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...