Wednesday, July 31, 2013

MFANYAKAZI WA KAMPUNI YA MWANANCHI APIGWA RISASI....YAINGIA NA KUTOKEA UPANDE WA PILI



Jessica Ngassa akimuhudumia mumewe, Jackson Ngassa ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Idara ya Usambazaji wa Magazeti aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi na majambazi Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam.

Watu ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi wamemjeruhi kwa risasi mfanyakazi wa Idara ya Usambazaji ya Mwananchi Communications Limited, Jackson Ngassa.
Tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi saa 4 usiku eneo la Tabata Matumbi baada ya watu hao kumfuatilia Ngassa tangu alipokuwa anatoka ofisi za Mwananchi eneo la Tabata Relini.

Akizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (Moi), Ngassa alisema wakati akitoka ofisini siku hiyo aliona pikipiki tatu zikiwa nyuma yake lakini hakuhisi kama zilikuwa zinamfuata mpaka walipofika taa za kuongozea magari za Tabata Dampo.

“Nilipofika Tabata Dampo nilihisi kufuatiliwa kwa sababu kila nilipopunguza mwendo nao walipunguza mpaka nilipofika Matumbi ndipo nikasikia wakiniambia simama haraka na kisha wakapiga risasi moja ambayo ilitoboa tanki la mafuta la pikikipiki,” alisema Ngassa.

Alisema baada ya kuona hivyo akataka kukimbilia Benki ya Access iliyoko eneo hilo la Matumbi lakini kabla hajafanya hivyo pikipiki nyingine ilimzuia kwa mbele na ghafla akasikia risasi ambayo ilipasua sehemu ya goti mguu wake wa kulia.

Hata hivyo, Ngassa alisema begi hilo halikuwa na pesa zozote zaidi ya kadi ya benki na magari ya kuchezea watoto aliyowanunulia watoto wake.

Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuunganisha mifupa iliyovunjika kwani risasi aliyopigwa iliingia na kutoka upande wa pili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari alikwishamtembelea majeruhi katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...