Serikali ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan chi hizo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
“Sasa ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani ili kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema Rais Obama.
Aliongeza kuwa pia ushirikiano huo unapaswa kuboresha utoaji wa mizigo katika bandari ya Dar es salaam na Mombasa kwenda nchi zisizo na bandari ili kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini.
Akizungumzia hotuba ya Rais Obama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini (CTI) Felix Mosha alipongeza hotuba hiyo kwa kufungua ukurasa mpya kwa nchi za Afrika na Marekani kwa kuonyesha kuwa wakati wa kutegemea misaada umepitwa na wakati badala yake ni kushirikiana katika uwekezaji.
Katika mkutano huo kiasi cha wafanyabiashara 170 walihudhuria mkutano huo .
No comments:
Post a Comment