Tuesday, July 2, 2013

KINYAMBE HATAKI KUISHI DAR



James Kinyambe mchekeshaji mahiri Bongo.

MCHEKESHAJI anayetamba katika tasnia ya filamu na vichekesho Bongo Mohamed Abdalah ‘Kinyambe’ amesema kuwa hata siku moja hajawahi kufikiria kuishi Dar es Salaam pamoja na watayarishaji wa filamu na vichekesho wakimlazimisha msanii huyo ahame Jijini Mbeya na kuishi Dar es Salaam kwani huko ndio kwenye kazi nyingi, lakini yeye anasema kwa sababu ana kitu pekee lazima waandaaji wamfuate..

James Kinyambe katika pozi lake.

James Kinyambe akiwa kazini.

“Sitaki kuishi Dar es Salaam kwa sababu naona kila msanii akikubalika na kuwa nyota lazima ahame kutoka mkoani na kuja Dar lakini ninajua ninachofanya, nashukru wale wanaojua uwezo wangu Star gani mimi ndio ninayewakilisha Mkoa wangu itokee siku mtu anataka kumuona Kinyambe aje Mbeya, tufanye kazi kuliko sote kujazana Dar es salaam,”anadai Kinyambe.

Aidha Kinyambe amesma kuwa soko kubwa la filamu na vichekesho lipo Dar es Salaam anaamini akiishi Jijini soko lake litashuka na kuonekana kama ni msanii wa kawaida tu kwa sababu anaonekana kirahisi kam ilivyo kwa wasanii wengine kwa sababu wanapohitaji muda wowote wanapatikana lakini kwake hata ukitaka kumwarika katika sherehe ya mtoto wako anafanya sherehe ya kuzaliwa utoe nauli aje kutoka Mbeya kama haujajipanga utashindwa.

Kinyambe ndio mchekeshaji anayependwa sana kwa sasa na kuwa na wapenzi wengi wa kazi zake, msanii huyo aliibuliwa na Al Riyamy Production jijini Mbeya na kuwa nyota.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...