Wednesday, June 12, 2013

KALA JEREMIAH KUMUENZI MANGWEA KWA MOJA YA TUZO ALITOZIPATA


Kala Jeremiah
Marehemu Mangera 
Msanii aliyeng'ara kwenye tuzo za Kili Awards Kala Jeremiah ameamua kumuenzi marehemu Mangwea kwa moja ya tuzo alizozipata, Kala ameyasema hayo kupitia  ukurasa wake wa facebook . soma alichoandika hapa:
TUZO YANGU MOJA YA MSANII BORA WA HIP HOP NIMEMPA ALBERT MANGWEA. HII NIMEIFANYA KWA AJILI YA KUDUMISHA MUZIKI WA NGWEA LAKINI PIA KUONYESHA KUWA HARAKATI ZA NGWEA HAZIJAKUFA BADO ZIKO HAI KWA KUWA MIMI NAAMINI HARAKATI HUWA HAIFI.

TUZO HII NAIPELEKA KESHO NIKISINDIKIZWA NA WASANII KADHAA NA WADAU WA MUZIKI.TUZO HII ITAFIKA ALIPOLALA HAYATI ALBERT MANGWEA NA ITAPOKELEWA NA MAMA YAKE MZAZI. NA ITAISHI NDANI YA NYUMBA YA MAMA YAKE KWA UKUMBUSHO WA MCHANGO WAKE KATIKA MUZIKI WA HIP HOP

KAMA WEWE NI MDAU WA MUZIKI NA UNGEPENDA KUAMBATANA NA SISI TUJUZE KWA NAMBA HII 0756799877 MIMI NITAGHARAMIA USAFIRI TU WA KWENDA NA KURUDI MAMBO MENGINE UTAJITEGEMEA. NA PIA NI LAZIMA UWE NA CHOCHOTE CHA KWENDA KUMUACHIA MAMA YETU. MAMA ALBERT.

MWENYEJI WETU AFANDE SELE NAYE ATAKUWA NA WATU KADHAA WATAKAOIWAKILISHA MORO.

KUMBUKA SAFARI HII TUNAENDA NA KUGEUZA KESHO HIYO HIYO

NA HAKUTAKUWA NA ONYESHO AU SHOW YA AINA YOYOTE KWA KUWA TUNAENDA MSIBANI.

ASANTENI SANA

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...