Mambo yamwendea mlama msanii kutoka Tanzania Mr.Nice ambae alikuwa ameula katika nchi jirani ya Kenya kwa kusaini mkataba mnomo na familia kubwa ya Muziki ya GrandPa Records inayowapeleka mbele sana wasanii kadhaa akiwemo DNA, Ng’ang’a wa TPF na wengine.
Mr. Nice amepigwa chini na Familia hiyo ambayo tayari ilikuwa imeshampigisha hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kumuandalia tour ya kumtambulisha nchi nzima kwa lengo la kumuongezea mashabiki, kumpa show ya kumtambulisha na kuachia ngoma moja aliyofanya na DNA “Tafuta”.
Grandpa Records kupitia C.E.O wao bwana Refigah wametoa tamko rasmi ambalo limetaja sababu za kumtema ikiwa ni pamoja na kuwa ni msanii huyo alikuwa ameshasaini mkataba na studio za Fishcrab chini ya Lamar na Sallam Sharaf na wakati anasaini mkataba na Grandpa Records hakuweka wazi.
Kupitia tamko hilo Grandpa Records wamemuelezea Mr.Nice kama msanii mvivu, asiye na ushirikiano, asiyetegemewa na mgumu kuliko wasanii wote waliowahi kufanya kazi chini ya Familia hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa ghafla, baada ya tamko hilo kufikia vyombo vya habari, C.E.O wa Grandpa Records aliitwa studio za Citizen radio na kufanya mahojiano na mtangazaji maarufu Willy M. Tuva kuelezea kwa undani sakata hilo, na mtangazaji huyo alipompigia simu Mr.Nice ili kupata maelezo kwa upande wake pia aligeuka mbogo na kutoa maneno kwa hasira akitishia kumbomoa mtu, na kwamba yeye sio wale wa ‘nyenyenyenyee’, msitari wa wimbo wa GrandPa family ‘Fimbo ya Pili’.
Hili ndilo tamko lililotolewa na GrandPa Records:
“To Grandpa Records fans and friends we've decided to drop Mr nice from Grandpa Records artists' roster. Mr Nice has been terminated for violating the agreement we entered with him.
For the sake of media and the general public we will summarize and say this, Mr Nice is the most difficult, uncooperative, lazy, unreliable artist we've ever worked with. The points and incidents of conflict are too many to mention here.
To be brief Mr Nice had previously signed a deal with Sallam Sharaf and Lamar in Tanzania and did not disclose this to us at the point of being signed to grandpa records. All in all, aluta continua we tried our best but he failed us.”
No comments:
Post a Comment