Wolper Gambe mwigizaji wa filamu
MWIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu Jaqueline Wolper amedai kuwa amefungua mwaka kwa kubadilisha jina toka la awali hadi kujiita Wolper Gambe jina ambalo anataka liwe alama yake kwa kila kitu atakachofanya atakitambulisha kwa jina hilo, pengine watu wengi walifikiria uenda jina lake jipya linaendana na tabia ya kutumia pombe kwa kiwango kikubwa, lakini mwenyewe alikana.
Wolper Gamba aka Jack akiwa katika pozi.
Wolper Gambe katika pozi
“Silewi na si mpenzi wa vileo lakini napenda muziki sana jina langu limetokana na muziki ambao naupenda sana ndio maana kwa sasa najiita Wolper Gambe ukiniita Wolper Gambe umefurahisha nafsi yangu kiukweli, watu wajua eti Gambe ni pombe hapana hizo ni swaga tu za sisi vijana, kitu kingine ninachopenda ni kumiliki gari nzuri,”anasema Wolper.
Aidha mwigizaji huyo alivyoulizwa kuhusu gharama ya gari yake mpya ya Mini Cooper alisema kuwa gari yake ni gharama kubwa lakini si rahisi kuitaja hadharani wakati kuna watu wana shida hawawezi hata kumiliki fedha ya kununulia chakula kidogo tu, msanii huyo ndio mwanamke pekee ambaye amekuwa akimiliki magari ya thamani kwa nyakati tofauti tofauti.
No comments:
Post a Comment