Wednesday, May 22, 2013

UJIO WA RAIS OBAMA NCHINI TANZANIA



Rais wa Marekani Bw. Baraka Obama na Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya nchi tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania, Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3 Julai.

Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.

Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa.
Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla

1 comment:

  1. Ujio wa Rais Obama ulenge katika kuwawezeshai wananchi wa Tanzania wanaoishi chini ya msitari wa umasikiki na usilenge kuwawezesha matajiri wafanyabiashara na viongozi wa nchi ambao hutoa ajira zenye mishahara midogo isiyoweza kumsaidia mwananchi katika kutatua matatizo madogo mfano matibabu na ukizingatia huduma hii inatolewa kwa garama ya juu ambayo mwananchi akupata ugonjwa anasubiri kifo kwani hushindwa kijitibu mwenyewe, pamoja na gharama nyingine muhimu kaka kusomesha watoto, umeme, maji na chakula. Vile vile ziara hiyo ilenge kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo katika kukuza miradi yao na makampuni ambayo hayana uwezo kuyapatia mtaji ili yaaweze kukua na kuendeleza uchumi wetu.....

    ReplyDelete

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...