
mwanamke alieuawa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi akiwa chini baada kupigwa risasi na watu hao kisha kuondoka na fedha kiasi cha shilingi milioni kumi alizokuwa nazo dada huyo(picha nablog ya wananchi)
Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi yamemuua kwa kumpiga risasi dada mmoja ambae hakufahamika jina lake mara moja kisha kuondoka na kiasi cha shilingi milioni kumi ambazo dada huyo alizichukua wakati akitoka benki ya CRBD tawi la uhuru jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea jana saa 11:16 jioni na watu hao inadaiwa walikuwa wanamfuatilia dada huyo kwa pikipiki kisha wakaligonga gari lake,alivyoshuka kuangalia kama gari limeumia,ndipo mmoja wa watu hao waliokuwa kwenye pikipiki akashuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokome na kiasi hicho cha fedha kusikojulikana.
Mpaka sasa hakuna taarifa yeyote kuhusu kukamatwa kwa watu waliohusika na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment