Thursday, May 9, 2013

DUCE YAPOKEA MSAADA WA KOMPYUTA 20 TOKA VODACOM FOUNDATION

Mkuu wa shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Prof David Mfinanga, akipokea msaada wa Kompyuta kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule zilizotolewa shuleni hapo eneo la Changombe Dar es Salaam jana, Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Vodafone Foundation kutoka India, Laura Turkington.

Mkuu…

Mkuu wa shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Prof David Mfinanga, akitazama moja ya Kompyuta alizokabidhiwa na Vodacom Foundation kama msaada katika harakati za kustawisha maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano shuleni hapo. Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo. Katikati ni Mkurugenzi wa Vodafone Foundation kutoka India, Laura Turkington na Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kushoto).
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi na Hisabati, Elizabeth Mrema, akitumia moja ya Kompyuta zilizotolewa na Vodacom Foundation shuleni hapo kama msaada Dar es Salaam jana, kushoto wanaomtazama ni Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule akiwa na baadhi ya wanafunzi. Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo, Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi na Hisabati, Anna Daniel, akitumia moja ya Kompyuta zilizotolewa kama msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo Dar es Salaam jana, kushoto wanaomtazama ni Maofisa wa Vodacom Foundation. Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo. Mkuu wa Kitivo cha Elimu wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo (kulia) akifafanua jambo mbele ya Maofisa mbalimbali wa Vodacom Foundation muda mfupi baada ya Kampuni ya Vodacom kupitia Mfuko wake wa Kusaidia Jamii kutoa msaada wa Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 kwa leongo la kustawisha matumizi ya Tehama shuleni hapo eneo la Chang'ombe Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...