Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Telesphor Mkude akiwa na mapadre na waumini wakielekea eneo la kutolea maombezi ya kumbukumbu ya kifo cha Sokoine
Jana Aprili 12, 2013 , Parokia ya Dakawa , wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro, ilifanya kumbukumbu ya Waziri Mkuu Hayati Marehemu Edward Moringe Sokoine kwa ibada ya misa takatifu iliyoendeshwa na Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, katika kanisa lilojengewa karibu na mahali alipofia baada ya kupata ajali ya gari Aprili 12, 1984 akitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam, sehemu alipofia hayato Sokoine ni Wami -Ruhindo,kilometa 40 kabla ya kufika mjini Morogoro na Kanisa alilojengewa na Jimbo Katolikila Morogoro linaitwa Kanisa la Picha ya Sokoine , tangu kufariki kwake dunia ametimiza miaka 29. Habari na picha na John Nditi.
Askofu Telesphor Mkude akiongoza sala ya maombezi ya kumwombea Marehemu Edward Sokoine baada ya kumalizika kwa ibada
Baadhi ya akina mama na watoto wao wakijumuika kanisani kumwombea Hayati Sokoine
Hapa ndipo alipofia aliyekuwa Waziri Mkuu , Edward Moringe Sokoine ,
Aprili 12, 1984 akitokea Mkoani Dodoma. Eneo hili ni Wami Ruhindo ,
kilometa 40 kabla ya kufika mjini Morogoro
Baadhi ya kina mama wa Jamii ya wamaasai wa Kijiji cha Wami Sokoine ,
wilaya ya Mvomero wakiwa nje ya kanisa wakati wa ibada ya mumwombea
marehemu Edward Sokoine
Kanisa laKatoliki Jimbo la Morogoro limejenga kanisa hili kumuenzi Hayati
Sokoine karibu na eneo alipopata ajali na kufariki dunia. Kanisa hilo
linaitwa Picha ya Sokoine
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka (wa pili kutoka kushoto)
na waumini wengine wakishiriki misa ya kumwombea Hayati Edward Sokoine eneo la Wami Sokoine.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( kulia) akifurahia jambo na
Askofu , Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro eneo la
Makao makuu ya Parokia ya Picha ya Sokoine
No comments:
Post a Comment