Friday, April 19, 2013

ADHABU YA SIKU TANO KWA WABUNGE WA CHADEMA HAITOSHI...WAFUKUZWE MIEZI MITATU".....HII NI KAULI YA MHADHIRI WA UDSM


Kitendo cha wabunge sita wa CHADEMA kufukuzwa juzi bungeni limezidi kuchukua sura mpya hapa nchini....


Wapo wanaodai kuwa adhabu hiyo haikuzingatia kanuni za bunge na badala yake ilitolewa kwa jazba za Naibu spika wa bunge.....


Mbali na hao, lipo kundi linaloamini kuwa adhabu hiyo ni sahihi na wanadai kuwa ni ndogo na pengine ingekuwa vyema kama ingeongezwa ili liwe fundisho kwa wabunge wengine


Kwenye kipindi cha tuongee asubuhi Star TV ,mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), Dr Bana, amesikika akisema kuwa adhabu waliopewa akina Lissu ya siku tano haitoshi na walitakiwa wapewe adhabu hata ya miezi mitatu na wakatwe mishahara pia.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...