Saturday, March 9, 2013

UHURU KENYATTA ACHUKUA KITI CHA URAIS NCHINI KENYA



Mchuano ulikuwa mkali kweli kweli, lakini hatimaye Uhuru Kenyatta ameibuka mshindi wa kinyang'anyiri hicho kwa asilimia 50.3 ya kura zote zilizopigwa huku Raila Odinga akijipatia asilimia 43.28 ya kura zote

RIPOTI KAMILI.....

MTOTO wa Rais wa kwanza wa Kenya, Marehemu Rais Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa anagombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TNA, Uhuru Kenyata ameshinda nafasi hiyo baada ya kumwangusha mpinzani wake Raila Odinga.


Hadi saa 8:35 usiku wa leo Uhuru alikuwa mbele kwa kura 6,173,433 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546 ikiwa ni tofauti ya kura 832,887 na majimbo yaliyo kwisha kutangazwa ni 291/291.


Jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni kura 12,338, 667 kutoka katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura zilizoharibika zikiwa 108975 na kura halali zikibaki 12,222,980.

Katika kinyang’anyiro hicho Wycliffe Musalia Mudavadi anashika nafasi ya tatu akiwa amejikusanyia kura 483,981 nafasi ya nne ikienda kwa Peter Kenneth mwenye kura 72,786.

Mgombea wa Alliance for Real Change,Mohamud Abduba Dida anashika nafasi ya tano akiwa na kura 52,848 akifuatiwa na Mwana mama Martha Karua wa National Rainbow Coalition mwenye kura 43,881 hadi sasa.
Nafasi ya saba katika wagombea hao Urais inakwenda kwa James ole Kiyiapi wa Chama cha Restore and Build Kenya ambaye ana kura 40,998 huku nafasi ya ya nane na mwisho ikishikwa na Paul Kibugi Muite wa chama cha Safina.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...