Tuesday, March 12, 2013

RAY, KING MAJUTO, JB NA IRENE UWOYA WATIKISA RWANDA.



Irene Uwoya mwigizaji wa filamu Sawhiliwood.

WASANII nguli katika tasnia ya filamu Swahiliwood Ray, JB, King Majuto na Irene Uwoya walikuwa gumzo katika tamasha la utoaji tuzo nchi Rwanda ambapo msanii kama Irene Uwoya ilibidi jina lake la asili lipotee na kujikuta akikumbushwa enzi za nyuma alivyotesa katika filamu iliyotamba na kuwa gumzo ya Oprah on Sunday.

Matangazo katika redio televisheni jina lilokuwa likisikika ni Oprah umugore wa Katawuti wakimananisha kuwa Irene mke wa mchezaji wa mpira Ndikumana, jina la Oprah limekuwa ni jina maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha wasanii nyota marehemu Steven Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’.

Wanyarwanda walilipuka ukumbi huku wakiita Oprah na Ray wakimwita Kigozi badala ya Kigosi, tuzo hizo zilizopewa jina la Rwanda Movie Awards zikilenga kuwatunuku wasanii wa filamu wa nchi hiyo na wasanii kutoka Bongo wakiwa kama watu mashuhuri waliofika kutoa zawadi kwa washindi walichaguliwa Rwanda Movie Awards.

Tamasha hilo la utoaji wa tuzo liliandaliwa na Ishusho Arts na kutoa mwariko kwa nyota wa filamu kutoka Swahiliwood, pia wasanii hawa waliweza kuona na viongozi wa nchi hiyo na kubadilishana mawazo kama wageni wanaowakilisha wasanii Afrika Mashariki.

JB akiteta jambo na Ray .


Ray akifuatilia utoaji wa tuzo za Rwanda Movie Awards.


King Majuto kwa nyuma na Ray , Irene Uwoya wakifuatilia kwa makini utoaji wa tuzo.


Irene Uwoya akifuatilia Rwanda Movie Awards kwa makini.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...