Friday, March 29, 2013

HIVI NDIVYO GHOROFA LILIVYOANGUKA POSTA JIJINI DAR.


Hiki ndicho kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15.

LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi Watanzania wameingia kwenye vilio baada ya jengo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es Salaam, kuanguka na kuwafunika watu waliokuwa eneo hilo na kusababisha wengine kupoteza maisha. Mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya watu waliokuwemo ndani yake, ila watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa.

Winchi likiokoa mabaki ya moja ya gari lililoangukiwa na kifusi.

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiangalia hali ya uokoaji inavyoendelea.
Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akitoa maelekezo ya jinsi ya kuondoa kifusi eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) akifuatilia shughuli ya uokoaji.
Watu mbalimbali wakiondoa kifusi.
Askari aliyejuu ya farasi akihakikisha usalama eneo hilo.
Baadhi ya watu wakilisukuma gari ambalo pia lilikuwa kwenye ajali hiyo.
Mama Salma Kikwete (kulia) na Rais Kikwete wakiangalia kifusi.
Kijana aliyenusurika katika ajali hiyo akinywa kahawa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...