Thursday, February 14, 2013

ROSE NDAUKA AKWAA SKENDO YA UTAPELI




Baada ya kuibuka kwa stori kibao mtaani zinazo muhusisha star wa filamu ndani ya bongo Rose Ndauka kuwa ni tapeli msanii huyo ameibuka na kuzungumza na sisi baada ya kimya kingi na stori kibao kuzagaa mtaani juu ya kuingia mitini na ‘mkwanja’ wa waigizaji wapya.

Sakata hilo limekuja mara baada ya msanii huyo kufanya usaili wa kutafuta vipaji vya wasanii wachanga kwa lengo la kuwachezesha filamu mara watakaposhinda katika usaili huo ambapo wasanii hao hununua fomu ya kujiunga.
 
Wakati na piga stori na msanii huyo ndipo nikapata ujumbe ulionijulisha uwepo wa kundi la wasanii waliofika kwenye ofisi zake zilipo maeneo ya Kinondoni Jijini Dar kudai fedha zao baada ya kushinda usaili uliofanywa na Rose na kuambulia patupu pasipo kushirikishwa katika filamu yoyote ya msanii huyo.

Tulimuuliza Rose na hapo ndipo alipofungua na kuweka wazi“Kaka nielewe Sijawahi kuchukua fedha ya mtu na kumnyima nafasi, kinachotokea ni tatizo la wasanii kukosa uvumilivu kwani si rahisi kumchukua kila mtu aliyeshiriki na kushinda usahili na kumuweka kwenye filamu, tunachokifanya ni kutoa nafasi moja kutokana na kipaji halisi kisha wengine wanafuata, lakini ajabu naona wengine wanalalamika bila kuelewa lakini sijawahi kula hela ya mtu” alisema Rose.Mtando huu uliwasiliana na mmoja wa wasanii hao ambaye alijitaja kwa jina moja tu la Krish na kusema kuwa,,Mimi binafsi pesa yangu ataitowa yeye si anajifanya mjanja hapa kafika anatataka kututapeli sisi alihoji msanii huyo n kuongeza kuwa kama hatarudisha pesa zao watampandisha mahakamani kwa kuwatapeli.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...