Saturday, February 9, 2013

"PENZI LA NISHA NA NEY WA MITEGO CHALI






MWANADADA anayeuza nyago kwenye soko la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amedai kuwa amekoma kuzoazoa wanaume bila kufanya uchunguzi.

Nisha alimwambia mwandishi wetu kuwa, amekuwa akiingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume mbalimbali bila kuwachunguza na matokeo yake imekuwa ni kuchezewa kisha kutoswa.

“Hii tabia ya kuzoazoa wanaume bila kuwachunguza inabidi niiache, mwanaume ambaye nitakuwa naye kuanzia sasa ni yule ambaye nitakuwa nimejiridhisha kuwa ananipenda kwa dhati. Kinyume chake bora niwe singo...” alisema Nisha.

Msanii huyo aliongeza kuwa kuna wanaume wanampotaka msichana hasa staa, hutumia gia ya kuoa lakini wakikubaliwa kisha kutoa penzi huingia mitini ndiyo maana ameamua kuwa makini na suala hilo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...