Friday, February 15, 2013

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MWAMINI MALEMI ALITAKA JESHI LA MAGEREZA KUONGEZA KASI ZAIDI KWA KUZINGATIA UWIANO WA JINSIA KATIKA UTEUZI WA VIONGOZI.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza na maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza kabla ya kufunga mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Malemi licha ya kulipongeza jeshi hilo kwa hatua nzuri ya kuwateua maafisa mbalimbali wanawake, alilitaka jeshi hilo kuongeza juhudi zaidi kwa kuwapa nafasi ya uongozi wanawake ambao wana uwezo na sifa ya kuongoza.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akimsalimia Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta (Kulia) wakati alipokuwa anawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya Jinsia kwa maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa.


Maafisa Magereza wakiifurahia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi alipokuwa anatoa hotuba ya kufunga mafunzo ya jinsia yaliyokuwa yanafanyika mjini Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu Mwamini Malemi (wa pili kutoka kulia) akimpa zawadi askari wa Jeshi la Magereza kutoka Gereza la Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi, Beatrice Sabo kwa kuwasilisha vizuri mada ya jinsi na jinsia wakati wa mafunzo hayo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Anayefuata ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta. Kulia ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Asina Omari.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...