Thursday, February 7, 2013

H.BABA ATOA TAMKO JUU LA BIFU LA FLORA MVUNGI NA SHILOLE!


MSANII wa miondoko ya bongo fleva H.Baba ameamua kufunguka juu ya malumbano yaliyotokea kwa wasanii wawili wa filamu nchini Shilole na Flora Mvungi,na kuelezea hatua ambazo amezichukua kuhusu malumbano hayo.

Akiongea na safu Maisha H.Baba alisema kuwa hatua ambayo ameichukua ni kumshauri mkewe mtarajiwa Flora Mvungi kuachana na malumbano na kuendelea na kazi zake kwani wanamajukumu mazito yanayowakabili

Alisema kuwa ameamua kumshauri hivyo kwa sababu tabia ya mke wake na malumbano ni vitu ambavyo haviendani naye na kutokana na majukumu na heshima ambayo anayo kwa jamii hapaswi kufanya hayo

"Unajua mke wangu hapaswi kulumbana lumbana hovyo kutokana na hadhi yake ambayo anayo kwa jamii hivyo kwa sasa lazima anisikilize mimi nilichomshauri na kutulia ili mambo mengine yaendelee"

Flora anajiandaa kutoa single nyingine hivi karibuni ambapo jina la nyimbo hiyo halijawekwa wazi.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...