Thursday, January 17, 2013

Nguvu ya kuzungumza ukweli; kupambwa na wasanii wakati wa tamasha la Sauti za Busara.



Khaira Arby (Mali).


Tamasha la Muziki la Sauti za Busara kwa mwaka huu litafanyika eneo la mji mkongwe Zanzibar, kuanzia tarehe 14 hadi 17 Februari, jitihada zimefanyika katika kufanikisha tamasha la 10 na kuhakikisha kuwepo kwa uhuru wa kujieleza kupitia nyimbo mbalimbali za wasanii wa Kiafrika ambao nyimbo zao zimepigwa marufuku au kuzuiwa katika nchi wanazotoka.

Kutakuwa na waimbaji wengi mahiri, akiwemo muimbaji mwenye misimamo kutoka jamii ya kiisilam nchini Mali, anaejulikana kwa jina la Khaira Arby ambae alifungiwa kuimba licha ya kwamba nyimbo zake zinamsifu/ elezea Mtume Mohammad (SAW). Mwengine ni Comrade Fasto anayetoka Zimbabwe, msanii mahiri wa kurap na mshauri, ambae nyimbo zake zinakosea serikali ya Mugabe hali iliyopelekea nyimbo zake kutopigwa katika radio na Televishen ya taifa. “Tuna uwezo wa kufikisha ujumbe wetu kwa walengwa. Tuna timu nzuri( mitaani) zenye uwezo wa kusambaza kopi nyingi za albam katika maeneo mbalimbali na hata katika mabasi ya abiria ambayo mengi yanatumiwa na wazimbabwe wa kawaida. Tumebuni njia mbadala “Radio Watu” na albam imekuwa zikichezwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri”. Alisema Comrade Fasto.

Wakati wa kongamano lijulikanalo kama Movers & Shakers ya Sauti za Busara, jopo la wasanii litafanya majadiliano ya kuangalia umuhimu wa kulinda uhuru wa kujieleza kwa wasanii. Nae Rebecca Corey, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions anaamini kwamba ni muhimu kwa wasanii kupata nafasi ya kupaza sauti zao. “Muziki ni njia moja yenye nguvu, lazima tuseme hali ya kutokuwa na usawa, tufurahie maisha, na kueleza hali ya utu wa mtu. Uhuru wa kujieleza ni haki za binadamu, na unatunufaisha sote ikiangaliwa na kuheshimiwa. Ndio maana Sauti za Busara ina jivunia kukuza sauti za wasanii kama Khaira Arby na Comrade Fasto ambao wamepigwa marufuku katika nchi wanazotoka”.

Msanii Khaira Arby kutoka Mali atafanya onesho lake katika tamasha la 10 la Sauti za Busara siku ya mwisho ya tamasha litakaloanza tarehe 14 hadi 17 Februari pale Ngome Kongwe, Zanzibar. Akivutiwa na binamu yake Ali Farka Toure, Khaira Arby katika muziki wake ameweka vionjo vya chimbuko la Berber na Songhai ambapo umekuwa ukileta mchanganyiko mzuri wa kuvutia wa desert blues na wakati wa kurikodi huchanganya na kinanda cha guitar la umeme, ngoni, ngoma na muziki wa kitamaduni na kuufanya mziki wake uvutie sana. Arby, amezaliwa katika kijiji ambacho hakipo mbali na mji wa Timbutku, ambao umezungukwa na jangwa.



Kwa upande mwingine, Samm Farai Monro, anaejulikana zaidi kama Comrade Fatso, ni mmoja wa msanii ambae ni maarufu na anavuma kwa mashairi Zimbabwe. Anaimba mashairi ya Toyi Toyi, mashairi ya mtaani yenye msimamo ambayo anachanganya na lugha ya Shona na kiingereza na mbira pamoja na hip hop. Atafanya onyesho lake sambamba na kundi la Tanzania Mlimani Park Orchestra wajulikanao pia kama Sikinde, Atongo Zimba kutoka Ghana, N’Faly Kouyaté kutoka Guinea, Owiny Sigoma Band kutoka Kenya, pamoja na wazimbabwe wenzake Mokoomba.

Miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania watakao shiriki katika tamasha la mwaka huu ni pamoja na Msafiri Zawose na Sauti Band, Lumumba Theatre Group, Super Maya Baikoko, Peter Msechu na wengineo wengi..

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...